Entertainment

Karma Ivien asaini mkataba wa kufanya kazi na msanii mkongwe Aziz Azion.

Karma Ivien asaini mkataba wa kufanya kazi na msanii mkongwe Aziz Azion.

Meneja wa wasanii kutoka Uganda Karma Ivien ameripotiwa kuingia ubia wa kufanya kazi na msanii mkongwe Aziz Azion.

Chanzo cha karibu na Aziz, kimesema karma tayaari amesaini mkataba wa kufanya kazi na msanii huyo ambapo anatarajiwa kusimamia kazi zake za muziki kama meneja.

Aziz Azion amekuwa akisuasua kimuziki kwa muda mrefu lakini kutokana na hatua ya kuhamua kufanya kazi na ivan karma wadau wa muziki uganda wamemtabiria mema kuwa huenda akatusua tena kisanaa.

Utakumbuka Ivan Karma ni moja kati ya wasimamizi wa wasanii ambao wamechangia mafanikio ya wanamuziki wengi nchini Uganda akiwemo Pallaso, Fik Fameica, VIP Jemo,Grenade na wengine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *