LifeStyle

Kauli ya Vera Sidika Yazua Hisia Tofauti Mitandaoni Kuhusu Wivu wa Wanaume

Kauli ya Vera Sidika Yazua Hisia Tofauti Mitandaoni Kuhusu Wivu wa Wanaume

Sosholaiti maarufu na mfanyabiashara Vera Sidika amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa kauli yenye utata kuhusu baadhi ya wanaume wa Kenya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vera alidai kuwa wapo wanaume wanaowaonea wivu wanawake, hasa wale waliofanikiwa, na hata baadhi yao kuwa na wivu kwa wake au wapenzi wao.

Kulingana na Vera, hali hiyo ya wivu inachangia matatizo mengi katika mahusiano ya kimapenzi. Aliongeza kuwa baadhi ya wanaume hushindwa kuvumilia mafanikio ya wake au wapenzi wao, jambo ambalo hupelekea migogoro na hata kuvunjika kwa mahusiano

“Some Kenyan men are jealous of women, especially successful women. Some men are even jealous of their own girlfriends, wives. Yes, it happens. There’s jealousy in relationships btw.” Aliandika

Kauli hiyo imeibua maoni tofauti kutoka kwa wafuasi wake na wanamitandao kwa ujumla. Baadhi wameunga mkono hoja hiyo wakisema kuwa wivu wa wanaume kwa wake zao ni jambo linalotokea hasa pale mwanamke anapoonekana kujiendeleza zaidi kimaisha. Wengine, hata hivyo, wamekosoa kauli hiyo wakidai kuwa ni ya kuwakandamiza wanaume na kwamba wivu unaweza kuwapo kwa pande zote mbili katika uhusiano.

Vera Sidika, ambaye amekuwa kwenye uhusiano wa hadharani na kuzungumziwa sana kutokana na mtindo wake wa maisha wa kifahari, amekuwa pia akijitokeza mara kwa mara kuzungumzia masuala ya mahusiano, wanawake na mafanikio.

Vera Sidika amekuwa mstari wa mbele katika kujieleza waziwazi kuhusu masuala ya kijamii na ya kifamilia, huku akitumia jukwaa lake la mitandao ya kijamii kuzungumzia mada mbalimbali zinazohusu maisha, mahusiano, na mafanikio ya wanawake.