
Msanii wa muziki Bongofleva Kayumba ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Sweet Pain.
Sweet Pain EP ina jumla ya ngoma sita za moto na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Nadia mukami,na Marioo
EP hiyo ina nyimbo kama Bomba Remix,Mapenzi Yanauma, Baishoo,Move on, Coco na Nimegonga ambayo ni Bonus track.
Sweet Pain ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Kayumba tangu aanze safari yake ya muziki na Nimegonga ambapo inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mtandao wa kukisikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.