Gossip

Kennedy Rapudo Azima Tetesi za Kuachana na Amber Ray

Kennedy Rapudo Azima Tetesi za Kuachana na Amber Ray

Mpenzi wa sosholaiti maarufu Amber Ray, Kennedy Rapudo, ameamua kutoa ya moyoni kuhusu tetesi zinazosambaa mitandaoni kwamba ameachana rasmi na Baby Mama wake huyo.

Rapudo amesema uvumi unaoenea mitandaoni hauna mashiko, akiwataja wanaoendeleza madai hayo kama watu wasio na shughuli na wanaopenda majungu ya mtandaoni.

Mashabiki wamekuwa wakitaka kujua iwapo kweli penzi lao limefika kikomo, lakini kauli ya Rapudo imeashiria kuwa hana mpango wa kuthibitisha au kukanusha rasmi mustakabali wa uhusiano wao.

Kauli yake inajiri wakati ambapo tetesi zimekuwa zikisambaa kuhusu hali ya uhusiano wake na mama wa mtoto wake, sosholaiti Amber Ray. Kumekuwa na fununu kuwa huenda mahusiano yao yamevunjika, hasa baada ya Amber Ray kuonekana mara kadhaa akihudhuria shughuli mbalimbali akiwa peke yake, tofauti na ilivyozoeleka wakiwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *