Entertainment

KESI YA CARDI B KUWASHUSHIA KICHAPO WAHUDUMU WA CLUB KUSIKILIZWA LEO

KESI YA CARDI B KUWASHUSHIA KICHAPO WAHUDUMU WA CLUB KUSIKILIZWA LEO

Rapa kutoka Marekani Cardi B  yuko hatarini kufungwa miaka minne  jela kufuatia mashtaka mawili yanayomkabili,ya kuwapiga na kuwafanyia fujo wahudumu wawili wa club iitwayo Angels-Strip-Club

Mwaka 2018 Cardi B alikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa makosa hayo mawili lakini mwaka wa 2019 alikanusha kwenye mahakama kuu ya queens akiwa kizimbani kwa kumwambia hakimu kuwa hana hatia

Inadaiwa Cardi B alitoa maelekezo kwa wasaidizi wake kuwapiga wahudumu hao wawili wa klabu hiyo  na baadaye yeye pia alishiriki kutembeza kipigo, kurusha viti na kupasua chupa mara baada ya kusikia kuwa mmoja kati yao alitoka kimapenzi na mumewe Offset.

Hata hivyo usikilizaji wa kesi hiyo umepangwa kufanya oktoba 25, mwaka huu na endapo rapa huyo atakutwa na hatia ya makosa yote mawili basi kifungo cha miaka minne  jela kitamhusu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *