Entertainment

Khaligraph Ageuza Kejeli Kuwa Faida Kupitia OG Omollo Sweatpants

Khaligraph Ageuza Kejeli Kuwa Faida Kupitia OG Omollo Sweatpants

Msanii wa Hip Hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonyesha ubunifu na ujasiri kwa kugeuza kejeli alizopokea kutoka kwa rapa Octopizzo kuwa fursa ya biashara.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Khaligraph alizindua Limited Edition OG Omollo Custom Sweatpants, hatua iliyowaacha mashabiki wake wakimpongeza kwa uamuzi wa kipekee.

Khaligraph ambaye anafanya vizuri na single yake mpya “Confuse” amehitimisha ujumbe wake kwa kutumia hashtag maarufu #respecttheogs, ishara ya kuendeleza msimamo wake wa kudumisha heshima na ushawishi katika anga ya muziki wa rap nchini humo.

Uamuzi huo ulionekana kama jibu la moja kwa moja kwa kejeli kutoka kwa rapa mwenzake, Octopizzo, ambaye alinukuliwa akisema “Kuna rapper flani huvaa sweatpants from January to December na timber ya yellow.”

Badala ya kuchukua maneno hayo kwa njia hasi, Khaligraph aliuchukua mtindo huo na kuubadilisha kuwa bidhaa ya kibiashara, hatua iliyotafsiriwa na mashabiki kama “clap back” ya kishujaa. Mashabiki wengi walimsifu kwa ubunifu huo, wakisema ni mfano bora wa jinsi msanii anaweza kutumia ukosoaji kujinufaisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *