Entertainment

Khaligraph Ajibu kwa Utani Madai ya Kuigiza Maisha na Muziki

Khaligraph Ajibu kwa Utani Madai ya Kuigiza Maisha na Muziki

Msanii nyota wa hip hop nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameonekana kuguswa na kauli za mtangazaji Rapcha the Sayantist, aliyemshutumu vikali kwa kudai kuwa muziki wake na maisha yake yote ni ya kuigiza.

Katika kujibu lawama hizo, Khaligraph ametumia ukurasa wake wa Instagram kwa mtindo wa utani, akionekana kugeuza matusi hayo kuwa fursa ya kumsaidia Rapcha kupata umaarufu zaidi. Amesisitiza kuwa kutajwa kwake ni njia rahisi ya kupata kiki, na akaenda mbali kwa kuwahimiza mashabiki wake wamfuate Rapcha mitandaoni.

Pia ametoa dondoo kwamba anajiandaa kuachia freestyle mpya, hatua ambayo mashabiki wameihusisha na majibu ya muziki kwa ukosoaji aliopewa.

Mashabiki mitandaoni wamegawanyika, baadhi wakiona kuwa Khaligraph ameonyesha busara kwa kutochukua mambo kwa hasira, huku wengine wakimtuhumu Rapcha kwa kutumia lugha ya matusi na kushusha heshima ya moja ya wasanii wakubwa zaidi wa hip hop Afrika Mashariki.

Hayo yote yameibuka mara baada ya Rapcha kwenye moja ya Podcast kudai kuwa kila kitu kuhusu Khaligraph ni cha kubuni kuanzia lafudhi yake, madai ya kutoka Kayole, mtindo wa mavazi hadi muziki anaoutoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *