Entertainment

Khaligraph Azidisha Bifu na Rapcha Kupitia Diss Track

Khaligraph Azidisha Bifu na Rapcha Kupitia Diss Track

Rapa Khaligraph Jones, ameonekana kuongeza moto kwenye bifu yake na podcaster na mchekeshaji Rapcha The Sayanist baada ya kuachia kipande cha diss track kupitia mitandao ya kijamii.

Katika kipande hicho cha distrack, Khaligraph anasikika akimrushia maneno mazito Rapcha, akidai vichekesho vyake ni vya kulazimisha na havina ubunifu wa kweli. Aidha, rapper huyo anadai Rapcha hana mafanikio ya kifedha ambapo ameenda mbali zaidi na kusema alihusika kuvunja uhusiano kati ya Rapcha na rafiki yake wa muda mrefu, Mwafreeka, ambaye pia ni muasisi wa Iko Nini podcast.

Bifu kati ya Papa Jones na Rapcha inadaiwa kuanza mwaka 2025 wakati Rapcha alipomkosoa Khaligraph hadharani, akimuita rapper bandia kwa kudharau mtindo wake wa mavazi. Rapcha alidai kuwa Khaligraph hana taste ya mavazi na mara nyingi huonekana akiwa amevalia sweatpants pekee.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *