Mtangazaji na mdau wa burudani mwenye utata, Mwijaku, amedai kuwa Kajala Masanja hana maisha wala mwelekeo wa kibiashara bila uwepo wa msanii wa Bongo Fleva, Harmonize.
Kwa mujibu wa Mwijaku, kipindi ambacho Kajala alikuwa nje ya mahusiano na Harmonize, maisha yake yalidorora kwa kiwango kikubwa, akidai kuwa alifilisika kiuchumi na kukosa kabisa dili za kibiashara. Anasema hakukuwa na brand wala kampuni zilizokuwa tayari kufanya kazi naye hadi pale aliporudiana na Harmonize.
Mwijaku ameongeza kuwa licha ya Kajala kutoka kimapenzi na wanaume wengi , hakuna mafanikio ya maana aliyoyapata kutokana na mahusiano hayo. Kwa mujibu wake, kile pekee ambacho Kajala anaweza kujivunia ni kusafiri nje ya nchi na kula bata kwenye mahoteli ya kifahari, mambo ambayo, kwa mtazamo wake, hayajengi msingi wa maisha yenye tija wala heshima ya kibiashara.