Entertainment

KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

KHALIGRAPH JONES AFUNGUKA VIGEZO VYA KUFANYA NAYE KOLABO

Rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones ametaja vigezo anavyotumia kumchagua msanii wa kufanya nae na kolabo.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Papa jones amesema yeye huwa angalii ukubwa wa msanii wala idadi ya wafuasi alionao kwenye majukwaa ya kustream muziki mtandaoni bali uzingatia sana ubunifu na kipaji cha msanii husika anapotaka kufanya kolabo.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Champez” amesema hata wasanii aliowashiriki kwenye album yake ya “Invisible Currency” ni watu ambao wana ukaribu nae na hivyo angemshirisha msanii ambaye hana uhusiano mzuri nae kwenye album yake hiyo.

Utakumbuka kwa sasa Khaligraph jones anafanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni kupitia Invisible Currency album ambayo inazaidi ya streams laki 5 kwenye mtandao wa Boomplay Kenya tangu iingie sokoni machi 17 mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *