
Mkali wa muziki wa hiphop nchini Khaligraph Jones amehamua kumpa Scar Mkadinali maua yake akiwa hai, kwa kumtaja kama mwaandishi bora wa nyimbo kwa upande wa wasanii wa hiphop nchini Kenya.
Akizungumza kwenye listening party ya album yake mpya Papa Jones amesema Scar anastahili kupewa heshimu hiyo kwa sababu anaitendea haki kiwanda cha muziki nchini.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Hiroshima amesema anafurahia mafanikio ambayo wasanii wa kundi la Wakadinali wamepata kwenye muziki wao ambapo am
meenda mbali zaidi na kusema kwamba anashangazwa na watu wanaomshindanisha na wasanii wa kundi hilo ikizingatiwa kuwa yeye ndiye aliwakutanisha na prodyuza Big Beats mwaka wa 2012, kipindi ambacho walikuwa wanachipukia kwenye game ya muziki wa Hiphop nchini Kenya.
Sanjari na hilo Khaligraph Jones amemtaja Msanii Mejja kama moja kati ya wasanii wakarimu aliowahi kutana na kufanya kazi nao.
Kwa sasa Khaligraph Jones anafanya vizuri na Album yake ya Ngoma 17 za Moto ya “Invisible Currency” ambayo inapatikana Exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay Kenya.