Entertainment

Khaligraph Jones aongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari

Khaligraph Jones aongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari

Rapa kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones ameongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari siku chache baada kurejea nchini akitokea Sierra Leone.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameposti video akiwa kwenye harakati ya kuosha ndinga yake mpya aina ya Lexus LX 570 huku akisindikiza na ujumbe unaosomeka “feels good to be back home”

Gari hiyo ya kifahari yenye thamani ya shilling million 12 za Kenya ni ya tano kuingia kwenye mikono ya Khaligraph Jones ikizingatiwa kuwa ana magari aina ya Subaru, Chrysler, Toyota Crown na Range Rover.

Ikumbukwe juzi kati Khaligraph Jones amekuwa nchini Sierra Leone ambako alienda kwa ajili ya ziara yake ya kimuziki ambapo alipata fursa ya kuwapa mashabiki zake burudani ya kipekee kupitia nyimbo zake tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *