Entertainment

Khaligraph Jones Atangaza Ujio wa Duka Kubwa la Mavazi 2026

Khaligraph Jones Atangaza Ujio wa Duka Kubwa la Mavazi 2026

Rapa kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones, ametangaza kuingia rasmi katika ulimwengu wa fasheni kwa mpango mpya unaotarajiwa kuvutia mashabiki na wadau wa mitindo.

Kupitia instastory yake, Rapa huyo amesema kuwa atazindua duka lake la mavazi na bidhaa za ubunifu mwaka 2026, hatua inayotafsiriwa kama mwanzo wa sura mpya katika safari yake ya kisanii na kibiashara.

Kwa muda mrefu Khaligraph amekuwa akionekana katika mavazi ya kipekee yanayoendana na taswira yake ya uhodari na ubunifu, na sasa anaonekana kutaka kugeuza muonekano huo kuwa biashara madhubuti.

Duka hilo litakuwa na mavazi ya kisasa, bidhaa za chapa yake na makusanyo yatakayoakisi mtindo wake wa kipekee unaojulikana na mashabiki wake.

Wadau wa muziki na mitindo wanasema huu ni wakati mwafaka kwa rapa huyo kuchukua hatua hiyo, kwani ushawishi mkubwa mitandaoni vinaweza kulifanya jaribio hili kufanikiw­a kwa kiwango cha kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *