Rapa mkali kutoka Kenya, Khaligraph Jones, ametikisa mitandao ya kijamii baada ya kuachia kionjo (teaser) cha ngoma yake mpya inayotarajiwa hivi karibuni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, rapa huyo amewashangaza mashabiki kwa kuposti video fupi akionekana anachana kwenye beat kali, akionyesha umahiri wake katika uandishi na utoaji wa mistari mizito.
Khaligraph amesindikiza video hiyo na caption iliyosomeka “USPIMEEEE MWANANGU”, kauli ambayo imetafsiriwa tofauti na mashabiki wake. Wengi wameichukulia kama ishara ya ngoma kali inayokuja, huku wengine wakidai ni ujumbe wa kuwachokoza wapinzani wake kwenye game ya rap.
Ndani ya muda mfupi tangu kionjo hicho kichapishwe, video imepokea maelfu ya likes na maoni, mashabiki wakimsifia kwa kurejea kwa kishindo kwa bars nzito. Baadhi walionekana kudokeza kuwa huenda ngoma hiyo ikawa sehemu ya mradi mkubwa unaotarajiwa kuachiliwa hivi karibuni.
Ingawa bado hajafichua jina la wimbo huo wala tarehe rasmi ya kuachiwa, wengi wanaamini Khaligraph anajiandaa kuachia ngoma kali itakayotikisa anga za muziki wa hip hop Afrika Mashariki.