
Rapa Khaligraph Jones amewachana baadhi ya wasanii wanaoishi maisha ya kuigiza yasiyokuwa na uhalisia.
Katika mahojiano yake na 2mbili Papa Jones amesema ni wakati wa mastaa na watu wenye majina makubwa kuacha kuishi maisha feki katika mitandao ya kijamii na badals yake wabuni vitu vya maendeleo kuliko kujionesha mitandaoni kuwa maisha yao ni bomba ilhali wanaishi kwa madeni
Aidha ameweka wazi kwamba mastaa wengi hujisukuma sana kuishi katika nyumba za kifahari na kumiliki magari makubwa kutokana na presha za mashabiki jambo ambalo amesema sio sawa kwa kuwa wanajidanganya wenyewe.
Khaligraph Jones ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wameonekana kutoogopa kukubali hali zao za kimaisha licha ya shinikizo kutoka kwa mashabiki.