Entertainment

KHALIGRAPH JONES AWEKA WAZI ALAMA ALIYOPATA KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KIDATO CHA NNE

KHALIGRAPH JONES AWEKA WAZI ALAMA ALIYOPATA KWENYE MTIHANI WA KITAIFA WA KIDATO CHA NNE

Rapa kutoka Kenya Khaligraph Jones amefunguka tusiyoyajua kuhusu maisha yake ya Elimu kwani ameamua kuweka wazi alama ambayo alipata kwenye mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne K.C.S.E.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Papa Jones amesema alipata alama ya D+ katika mtihani wake wa kitaifa baada ya kuacha shule kwa miaka mitatu kutokana na matatizo ya kulipa karo.

Hitmaker huyo wa ngoma ya Hiroshima amesema alihamua  kurudi shule ili awe mfano mwema kwa ndugu zake kwani alikuwa mtoto wa kwanza katika familia ya watoto sita kumaliza kidato cha nne.

Hata hivyo watumiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii wamempongeza rapa Khaligraph Jones kwa hatua ya kuweka wazi alama aliyopata kwenye mtihani wake wa kitaifa wakisema kuwa itawapa moyo vijana wengi waliokata tamaa maishani baada ya kufeli kwenye masomo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *