Entertainment

Khaligraph Jones Azindua Rasmi Rap Battle ya Wimbo Wake Mpya “Weyuat”

Khaligraph Jones Azindua Rasmi Rap Battle ya Wimbo Wake Mpya “Weyuat”

Msanii nguli wa muziki wa rap nchini Kenya, Khaligraph Jones, ameanzisha rasmi rap battle ya wimbo wake mpya “Weyuat” baada ya kupata shinikizo kutoka kwa mashabiki wake mitandaoni.

Khaligraph amesema awali hakupanga kufanya challenge hiyo, lakini mashabiki wake waliamua kuigeuza kuwa challenge rasmi. Amesema atapakia instrumental ya wimbo huo ili rappers wote wanaohisi wana uwezo waweze kuonyesha kipaji chao kupitia beat hiyo. Pia ameongeza kuwa endapo mambo yataenda vizuri, huenda wakafanya remix maalum ya wimbo huo.

Rapper huyo ameahidi kutoa nafasi sawa kwa washiriki wote, akisisitiza kuwa changamoto hiyo ni jukwaa la kuibua vipaji vipya katika muziki wa rap Afrika Mashariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *