
Siku chache baada ya kufanya shoo yake nchini Sierra Leone, Rapa Khaligraph Jones ametangaza show nyingine ya kimataifa nchini Australia mwishoni mwa mwezi huu.
Kupitia mitandao yake ya kijamii amesema anatarajia kufanya show zake kwenye miji ya Perth na Sydney, Januari 27 na 29 mtawalia.
“Whats good Australia, OG is coming through, January Friday 27th Perth and Sunday 29th Sydney,” Aliandika.
Khaligraph alitumbuiza mjini Free Town, Sierra Leone juzi kati ambapo aliwapa mashabiki zake burudani ya kufa mtu kupitia nyimbo zake zilizofanya vizuri kipindi cha nyuma.
Rapa huyo ameanza kufanya shows zake za kimtaifa baada ya kuachia wimbo wa “Avengers Cypher” ambao alimshirikisha rapa anayekuja kwa kasi nchini Katapilla, wimbo ambao unafanya vizuri kwenye mtandao wa Youtube.