Entertainment

Killy na Cheed waishtaki lebo ya Konde Music Worldwide kwa kuvunja mkataba wao

Killy na Cheed waishtaki lebo ya Konde Music Worldwide kwa kuvunja mkataba wao

Mambo yanazidi kuwa mengi baada ya wanamuziki Killy na Cheed kuondoshwa katika lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide ambapo wasanii hao wameripotiwa kufika Baraza la Sanaa Tanzania BASATA kwa madai ya kufuatilia na kukamilisha mchakato wa kuachana na lebo hiyo.

Meneja wa wasanii hao Sats Sembe, amesema sababu ya wao kufikisha malalamiko yao Basata ni kupinga utaratibu wa kuvunja mkataba na wasanii hao ambapo ameeleza kuwa hakuna barua yoyote ya maandishi waliopewa mpaka sasa.

Sembe amesema kwa kuwa waliingia lebo ya Konde kwa maandishi basi hata kuondoka wanapaswa kuondoka kwa maandishi, ili kesho isije kutokea sintofahamu katika masuala ya kisheria.

“Huko mbeleni hatujui hili suala litafika hapa, lakini kwa kuanzia tumeanzia kwa walezi wetu na wazazi wetu Basata ambao katika hali ya kawaida tusingeweza kuwaruka.

“Lakini kama ikishindikana hatua hii tutaeda hata mahakamani ambapo kote huku barua ya maandishi ni muhimu kama ushahidi kwamba wameachana na wasanii”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *