Entertainment

Kim Kardashian afunguka kuhusu imani yake kwa Mungu

Kim Kardashian afunguka kuhusu imani yake kwa Mungu

Mwanamitindo maarufu nchini Marekani Kim Kardashian amefunguka kuhusu imani yake kwa Mungu na jinsi anavyoshiriki jambo hilo na watoto wake.

Katika kipindi maalumu cha Angie Martinez IRL Podcast, Kardashian aliulizwa ikiwa huwa na kawaida ya kufanya maombi(anasali), alisema; “Mimi ninasali kila usiku na watoto wangu. Hata kama niko nje ya mji, lazima wanipigie simu, na tunasali pamoja kupitia FaceTime,” aliendelea.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 42 alisema mara nyingi anasali na kuomba kwa ajili ya Afya na furaha ya familia yake na alipoulizwa kuhusu maisha yake ya kimahusiano, alisema anaamini katika Mungu, upendo, imani katika yote, na anaamini Mungu atamletea mtu sahihi kwenye maisha yake.

Mnamo 2021, Kardashian aliomba talaka kutoka kwa rapa Kanye West, kufuatia miaka sita ya ndoa yao hii ikiwa ni ndoa yake ya tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *