
Msanii maarufu wa Kenya, King Kaka, ameonyesha furaha isiyo kifani baada ya kuhudhuria hafla ya tuzo za BET Awards 2025 iliyoandaliwa katika ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles, California.
Kupitia video aliyoipakia kwenye Instagram, ikimuonesha mwanamuziki wa kimataifa Lil Wayne akitumbuiza, King Kaka anaonekana kushangazwa na kuwa karibu sana na mastaa waliomtia motisha tangu akiwa mtoto, akisisitiza kuwa tukio hilo limemfungua macho na kumpa msukumo mpya katika safari yake ya muziki na maisha kwa ujumla.
“Sijawahi kuhamasika hivi maishani mwangu wote!!! Naahidi maisha yangu yamebadilika kabisa.
Kumbukumbu zote za utotoni ziko mstari wa nne kutoka hapa, hapa tu!!! Na bado tuna safari ndefu sana mbele yetu. Kwa njia, wewe unaona nani?,” King Kaka aliandika ujumbe uliogusa hisia za mashabiki wake.
Mashabiki wake walimpongeza kwa hatua hiyo, wakimtia moyo kuendelea kuwakilisha Kenya na Afrika Mashariki kwenye majukwaa ya kimataifa. Tukio hilo limeonekana kama ushahidi wa jinsi sanaa ya Afrika inavyozidi kutambuliwa kimataifa.