
Rapper kutoka Nchini Kenya King Kaka ametusanua kuwa album yake mpya imekamilika.
Mkali huyo wa ngoma ya “Fight” ameweka wazi hilo kwenye podcast ya jalang’o tv huku akiwataka Mashabiki zake wakae Mkao Wa Kuipokea Album Yake Mpya Itakayoingia Sokoni Hivi Karibuni.
Hata hivyo King Kaka hajatuambia idadi ya ngoma zitakazopatikana kwenye album hiyo wala tarehe rasmi ya album yenyewe kuingia sokoni ila ni jambo la kusubiriwa
Hii itakuwa ni album ya sita kwa mtu mzima wa King Kaka tangu aanze safari yake muziki ikizingatiwa kuwa tayari ana album tano, mixtape 9 na EP moja.