
Msanii wa Uganda, King Saha, ametoa onyo kali kwa Alien Skin akimtaka kuacha mara moja kumshambulia nyota wa muziki Jose Chameleone.
Akiwa jukwaani wakati wa moja ya shoo zake jijini Kampala, King Saha amesisitiza kuwa yuko tayari kupambana na yeyote atakayemvunjia heshima Chameleone, akimtaja kama mlezi na msanii ambaye ametoa mchango mkubwa katika sekta ya muziki wa Uganda.
Saha amesema licha ya changamoto au tofauti ambazo wakati mwingine zimekuwapo kati yake na Chameleone, heshima yake kwake haijawahi kupungua, na kwamba ataendelea kumtetea kila mara.
Onyo hili linakuja wakati ambapo Chameleone na kiongozi wa Fangone Forest, Alien Skin, wamekuwa wakirushiana maneno kwa siku kadhaa. Mzozo huo ulianza baada ya Chameleone kuubeza wimbo wa Alien Skin “Kapati” akisema hauna thamani, hatua iliyochochea vita vya maneno kati ya wawili hao.