
Inaonekana mwanamuziki kutoka nchini Uganda King Saha ameanza kuwa mtu mwema hii ni baada ya kukiri hadharani kuwa ameachana kabisa na matumizi ya mihadarati.
Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha amethibitisha kuacha kutumia madawa ya kulevya na badala yake amehamua kuelekeza nguvu zake zote kwenye suala la kuiweka mwili wake sawa na pia kuboresha muziki wake ambao umekuwa ukisuasua katika siku za hivi karibuni.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Sala Pulesa” amewashauri vijana kujitenga na masuala ya kutumia dawa za kulevya kwani matumizi ya dawa hizo ni hatari kwa maisha ya binadamu.
Utakumbuka mwaka wa 2020 Bebe Cool alimshauri King Saha aache suala la kutumia mihadarati kwani inaathiri kazi zake za muziki lakini msanii huyo hakupokea vyema ushauri huo ambapo alienda mbali zaidi na kumshambulia bebe cool kwa kusema kuwa anamuonea wivu hivyo hapaswi kuingilia maisha yake.