Gossip

King Tizian Anunua Audi S7, Asema Yeye Ndiye Mkenya wa Kwanza Kumiliki Gari Hilo

King Tizian Anunua Audi S7, Asema Yeye Ndiye Mkenya wa Kwanza Kumiliki Gari Hilo

Tiktoker kutoka Kenya, King Tizian ameibua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa yeye ndiye Mkenya wa kwanza kumiliki gari la kifahari aina ya Audi S7 4.0L V8 yenye thamani ya shillingi millioni 14.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, King Tizian ameshiriki picha na video akionyesha gari hilo la kifahari huku akieleza furaha yake kubwa akisema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya maono aliyoyaanza kama ndoto na sasa yamegeuka kuwa uhalisia

Audi S7 4.0L V8 ni gari lenye nguvu kubwa na hadhi ya juu, likijulikana kwa muonekano wake wa kisasa, kasi ya hali ya juu pamoja na teknolojia ya kiwango cha dunia. Hatua ya King Tizian kununua gari hilo inamuweka miongoni mwa vijana wanaoonyesha kuwa ndoto zinaweza kutimia kupitia juhudi, ubunifu na matumizi sahihi ya majukwaa ya kidijitali kama TikTok.

Wengi wamechukulia hatua hiyo kama motisha kwa vijana wengine kuamini maono yao na kuyafanyia kazi hadi yatimie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *