Entertainment

Kings Music Records Yafungua Ukurasa Mpya kwa Kumsajili Msanii wa Kike

Kings Music Records Yafungua Ukurasa Mpya kwa Kumsajili Msanii wa Kike

Lebo ya muziki Kings Music Records inayoongozwa na gwiji wa Bongo Flava Alikiba imemtambulisha rasmi msanii wake mpya Mutima Wangu, mwenye asili ya Rwanda, hatua inayofungua ukurasa mpya katika historia ya lebo hiyo.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mitandaoni, Alikiba ameeleza fahari yake kwa kumsajili msanii huyo wa kike, akisisitiza kuwa ni nyota mpya mwenye dhamira ya kudumu kwenye muziki wa Afrika na duniani.

Kutambulishwa kwa Mutima Wangu, Kings Music Records inaonekana kupanua wigo wake kimataifa huku ikitoa nafasi kwa vipaji vya kike kung’ara chini ya usimamizi wa mmoja wa wasanii wakubwa zaidi katika historia ya Bongo Flava.

Kwa sasa, macho na masikio ya mashabiki yako wazi kusubiri kuona ni aina gani ya muziki Mutima ataleta na jinsi atakavyoiwakilisha Rwanda na ufalme wa Kings Music kwenye ramani ya muziki wa kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *