Mwanamitandao mwenye utata kutoka Kenya, Kelvin Kinuthia, amefunguka kuhusu mpango wake wa kufanyiwa upasuaji wa kuboresha mwili wake baada ya safari yake ya kupunguza uzito kwa kutumia dawa za Ozempic kupata mafanikio.
Akizungumza kwenye YouTube channel yake, Kinuthia amesema kuwa anapanga kufanyiwa BBL (Brazilian Butt Lift) na tummy tuck, hatua ambazo ni muhimu baada ya kupunguza uzito kutoka kilo 146 hadi 70.
Kinuthia anayefahamika kwa kuvalia nguo za kike na kuunda maudhui ya kuchekesha Tiktok, amefafanua kuwa kupungua kwa uzito kiasi hicho kunaweza kuacha ngozi iliyolegea na upasuaji huo utamsaidia kupata muonekano wa kujiamini zaidi.
Katika ujumbe wake, Kinuthia amewapa motisha mashabiki wake, akisisitiza kuwa safari ya kupunguza uzito na mabadiliko ya mwili ni kwa ajili ya afya njema na kujiamini binafsi. Hata hivyo ameahidi kuwa ataendelea kuweka wazi maendeleo yake yote kwa wafuasi wake mtandaoni.