Kinuthia Atangaza Mpango wa Kufanya BBL na Tummy Tuck

Kinuthia Atangaza Mpango wa Kufanya BBL na Tummy Tuck

Mwanamitandao mwenye utata kutoka Kenya, Kelvin Kinuthia, amefunguka kuhusu mpango wake wa kufanyiwa upasuaji wa kuboresha mwili wake baada ya safari yake ya kupunguza uzito kwa kutumia dawa za Ozempic kupata mafanikio. Akizungumza kwenye YouTube channel yake, Kinuthia amesema kuwa anapanga kufanyiwa BBL (Brazilian Butt Lift) na tummy tuck, hatua ambazo ni muhimu baada ya kupunguza uzito kutoka kilo 146 hadi 70. Kinuthia anayefahamika kwa kuvalia nguo za kike na kuunda maudhui ya kuchekesha Tiktok, amefafanua kuwa kupungua kwa uzito kiasi hicho kunaweza kuacha ngozi iliyolegea na upasuaji huo utamsaidia kupata muonekano wa kujiamini zaidi. Katika ujumbe wake, Kinuthia amewapa motisha mashabiki wake, akisisitiza kuwa safari ya kupunguza uzito na mabadiliko ya mwili ni kwa ajili ya afya njema na kujiamini binafsi. Hata hivyo ameahidi kuwa ataendelea kuweka wazi maendeleo yake yote kwa wafuasi wake mtandaoni.

Read More
 Kelvin Kinuthia Atangaza Mpango wa Kufanyiwa Upasuaji wa Uterus Transplant

Kelvin Kinuthia Atangaza Mpango wa Kufanyiwa Upasuaji wa Uterus Transplant

Mshawishi wa mitandaoni kutoka Kenya, Kelvin Kinuthia, amewashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza kuwa ana mpango wa kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza mfuko wa uzazi (Uterus Transplant – UTX). Hii ni aina ya upasuaji wa kibingwa ambapo mfuko wa uzazi kutoka kwa mtoaji (donor) hupandikizwa kwa mpokeaji ili kumpa uwezo wa kubeba mimba Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza kwamba maisha yake ni ya faragha na hakuna aliyekuwa akifahamu mipango yake ya kufanyiwa upasuaji huo. Amesema amekuwa akipitia maandalizi ya kimatibabu kwa muda mrefu na amejiandaa kisaikolojia kwa safari hiyo. Pia amefafanua kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu anaamini kila mtu ana haki ya kuwa na familia na kupata mtoto, na ana matumaini makubwa kuwa teknolojia ya kisasa ya tiba itamwezesha kutimiza ndoto hiyo. Kwa mujibu wa Kinuthia, uamuzi wake wa kuzungumzia suala hilo hadharani unatokana na dhamira ya kuwapa ujasiri watu wengine wanaopitia changamoto za kiafya au wale wanaotamani kupata watoto kwa njia zisizo za kawaida. Uterus transplant ni miongoni mwa upasuaji wa hali ya juu unaofanyika mara chache duniani na umewezesha wanawake waliokuwa hawana uwezo wa kubeba ujauzito kupata nafasi ya kujifungua watoto wao wenyewe. Hata hivyo, upasuaji huu unahitaji maandalizi ya kina, usimamizi wa madaktari bingwa, na dawa maalum za kuzuia mwili kukataa kiungo kilichopandikizwa.

Read More