
Uongozi wa Lebo ya muziki ya Saldido International ukiongozwa na Willy Paul umetangaza kumalizika kwa mkataba baina yao na msanii Klons Melody.
Kupitia ukurasa wake Instagram, Willy Paul amemshukuru Klons Melody kwa uwepo ndani ya Saldido International katika kipindi cha miezi kumi, lakini pia amemtakia Kila la kheri na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano kwenye kazi zake.
Klons Melody alisainiwa na lebo ya Saldido International Mei 11, mwaka 2021 na kuachia kazi kadha ikiwemo Odi Love na Atoti Jaber.
Utakumbuka mwezi Novemba 21 Willy Paul alimsaini msanii wake iitwaye Queen P, miezi kadhaa baada ya msanii wake wa kwanza Miss P kujiondoa kwenye lebo hiyo.