Sports news

Kocha wa Gor Mahia Ataja Kocha Bora wa Ligi Kuu Mwezi Oktoba

Kocha wa Gor Mahia Ataja Kocha Bora wa Ligi Kuu Mwezi Oktoba

Mkufunzi wa Gor Mahia Charles Akonnor ametajwa kuwa kocha bora wa ligi kuu nchini mwezi wa Oktoba. Akonnor, ambaye anaifunza Gor Mahia kwa mara ya kwanza aliiongoza kunyakua ushindi mara tatu mtawalia dhidi ya KCB,Posta Rangers na Mathare United.

Msururu huo wa kutoshindwa uliiwezesha Gor kuchupa hadi kileleni pa msururu wa ligi kuu ambapo wanaongoza kwa alama 16, alama moja mbele ya Kakamega Homeboyz iliyo ya pili.Wakati uo huo ligi kuu nchini itaingia raundi ya kumi wikendi hii huku zikiwa zimepangwa kufanyika jumla ya mechi saba.

Hii leo Jumamosi,Gor Mahia itamenyana na Tusker Fc ilhali mabingwa watetezi Kenya Police watachuana na Mathare United, Bidco itakuwa nyumbani dhidi ya Bandari uwanjani Sportpesa Arena huku Mara Sugar ikiikaribisha KCB uwanjani Awendo.

Jumapili AFC Leopards itachuana na Kariobangi Sharks nayo Muranga Seal imenyane na Shabana FC uwanjani Sportpesa Arena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *