Content creator kutoka Kenya Mjaka Mfine amevunja ukimya na kukanusha madai yanayoendelea mtandaoni kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake aitwaye Mokaya.
Akizungumza katika mahojiano na Shiksha Arora, Mrembo huyo amefafanua kuwa madai hayo hayana msingi na kwamba uhusiano wao uko kwenye misingi ya kazi pekee.
Mjaka amesema kuwa yeye na Mokaya wamekuwa wakifanya miradi kadhaa ya pamoja, jambo ambalo limewachochea baadhi ya mashabiki kudhani kwamba wana uhusiano wa karibu zaidi ya kazi. Hata hivyo, amesisitiza kuwa ushirikiano wao umejengwa kwenye taaluma, ubunifu na malengo ya pamoja ya kimaudhui.
Utata huo umeibuka kutokana na kemistri inayodhihirika kwenye video zao, hali iliyowafanya baadhi ya wafuasi kufikia hitimisho kwamba wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi.