
Kocha Mkuu wa Gor Mahia, Charles Akonnor ameelezea imani na kikosi chake huku vigogo hao wa soka humu nchini wakitarajiwa kuchuana na wababe wa Tanzania, Simba SC katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa kwa msimu mpya kesho Septemba 10 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mechi hiyo inatarajiwa kuvutia maelfu ya mashabiki kutoka mataifa yote mawili ni ya kunoa tomi hizo kabla ya kung’oa nanga Kwa michuano ya ligi za nyumbani. Gor Mahia, ambao ni wabambe wa Ligi Kuu ya Kenya waliwasili Tanzania mapema wiki hii na wamekuwa wakiimarisha mazoezi yao.
Kocha mkuu Charles Akonnor, ambaye alichukua hatamu mapema mwaka huu anasema kikosi chake kiko tayari kushamiri. Michuano ya ligi msimu huu itang’oa nanga tarehe 20 mwezi huu.