
Mwanamuziki KRG The Don amejipata pabaya kwenye mitandao ya kijamii baada ya wakenya kumshambulia kwa madai ya kuwavunjia heshima kutokana na hatua ya serikali kuondoa ruzuku ya mafuta.
Kwenye ujumbe wake aliochapisha kwenye mtandao wa Instaram KRG aliwataka wakenya waache kulalamika kuhusu bei ya mafuta kupanda ikizingatiwa kuwa wengi wao hawamiliki magari yanayohitaji bidhaa hiyo muhimu.
Hakuishi hapo alienda mbali zaidi na kuwaponda wakenya kwa kusema kuwa kulalamika kwao kumewafanya watu kuhisi wanapitia maisha magumu wakati sio kweli.
“Unalalamika mafuta imepanda na hauna gari? Sisi watu tuko na 6.3L engine na German machines hatulalamiki. Unalalamika na unatembea na slippers yako na footsubishi? Nyinyi ndio mnafanya nchi ikae ni kama watu wanateseka na watu hawateseki.” Ameandika
Sasa ujumbe huo umeonekana kuwakera watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wameshushia kila aina matusi msanii huyo huku wakisema bei ya mafuta inamuathiri kila mkenya bila kuzingatia utajiri alionao.
Hata hivyo wamemalizia kwa kumtaka KRG The Don aanze kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji katika jamii kama kweli ana utajiri mkubwa badala ya kuisha maisha ya kuigiza kwenye mitandao ya kijamii.
Utakumbuka juzi kati Serikali ya rais William Ruto iliondoa ruzuku ya mafuta kwa sababu imekuwa haiwasaidii raia wa Kenya wanaoendelea kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha