Entertainment

KRG THE DON ADOKEZA KUANZA ZIARA YA MUZIKI NJE YA KENYA

KRG THE DON ADOKEZA KUANZA ZIARA YA MUZIKI NJE YA KENYA

Msanii wa dancehall nchini KRG The Don amefunguka tusiyoyajua kuhusu muziki wake.

Katika mahojiano yake hivi karibuni amesema alilazimika kusitisha ziara yake ya muziki nje ya Kenya kwa sababu migogoro iliyokuwa inazingira ndoa yake mapema mwaka huu.

Hitmaker huyo wa Ushasema amesema kwa sasa ametatua changamoto zilizokuwa zinamuandama kipindi cha nyuma, hivyo yupo mbioni  kuanza kufanya ziara yake ya kimuziki kimataifa.

Katika hatua nyingine amewachana wasanii wa nyimbo za injili nchini waache unafiki na badala yake waugeukia muziki wa kidunia ambao una pesa nyingi.

KRG amesema hayo alipotua nchini akitokea Sudan Kusini ambako alienda kutumbuiza kwenye moja ya show aliyokuwa amealikwa wikiendi hii iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *