
Mwanamuziki wa dancehall nchini Krg The Don ameamua kujitolea kumsaidia mwongozaji wa video nchini Tiger Mind Vision ambaye anadaiwa kuwa hana makaazi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Krg the Don amewataka watu walio na ukaribu na Tiger Mind Vision wawasiliane naye ili aweze kufanikisha mchakato mzima wa kumsaidia.
“Someone put me in contact wirth Dir, Tyga or Tell him to come to Casavera lounge from 4pm We see how we can help”, Ameandika instastory.
Kauli ya Bosi huyo wa Cash group Entertainment inakuja mara baada ya Picha za Tiger Motions kusambaa mtandaoni akiwa anaisha maisha ya uchochole kutokana na kukosa makaazi ya kuishi.
Utakumbuka Tiger Motion ni moja kati ya waongozaji wa video za muziki nchini aliyeacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini kupitia video za nyimbo kama Mama ya Bahati, Lala Salama ya Willy Paul, Ndio yako ya Gloria Muliro, Tenda Wema ya Ringtone na nyingine nyingi.