Entertainment

KRG THE DON AONYESHA JEURI YA PESA KWA MASHABIKI

KRG THE DON AONYESHA JEURI YA PESA KWA MASHABIKI

Msanii wa muziki wa dancehall nchini Krg The Don ameamua kutuonyesha jeuri ya pesa anazozitolea jasho kila kuchao kwenye shughuli zake za kibiashara.

Kupitia instastory kwenye mtandao wa instagram Krg ameshare taarifa ya mpesa yake inayoonesha kuwa ametumia kiasi cha shillingi millioni 10 za Kenya katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Katika taarifa yake hiyo amebainisha kuwa kwa wastani anatumia takriban millioni 1.6 kwa mwezi kwenye matumizi yake ya binafsi jambo ambalo limezua gumzo mtandaoni miongoni mwa wakenya.

Hata hivyo watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemtaka Krg The Don aache kuwapotosha vijana kwa kuwafanya wajiingize kwenye visa vya uhalifu kwa ajili ya kujipatia kipato huku wengine wakionekana kumtolea uvivu msanii huyo kwa madai ya kutumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *