
Msaniii Krg the Don ametoa angalizo kwa mashabiki zake kutofuata au kuamini kile anachokiweka mtandaoni.
Katika mahojiano hivi karibu bosi huyo Cash Group Entertainment amesema hayuko mtandaoni kuwafurahisha au kuwashauri watu, hivyo wasichukulie kwa uzito kila kitu anachokiandika mtandaoni kwani inaweza kuwasababishia matatizo.
Kauli ya Krg The Don imekuja mara baada ya watu kumkosoa mtandaoni kufuatia kitendo chake cha kuweka hadharani taarifa ya mpesa yake inayoonesha kuwa ametumia kiasi cha shillingi millioni 10 za Kenya katika kipindi cha miezi sita iliyopita.
Hatua hiyo ilikosolewa na wengi wakimtaka Krg The Don aache kuwapotosha vijana kwa kuwafanya wajiingize kwenye visa vya uhalifu kwa ajili ya kujipatia kipato.