
Mwanamuziki wa Dancehall kutoka Kenya, KRG The Don amezindua programu ya simu inayojihusisha na michezo ya kubashiri iitwayo Maisha POA App, inayolenga kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Katika mkao na wanahabari KRG The Don amesema app hiyio ambayo inapatikana Google Playstore kwa watumiaji wa mfumo wa Android itatoa fursa kwa vijana kujishindia shillingi millioni 1.2 kwa siku.
Msanii huyo amesema mtumiaji atatakiwa kulipa shillingi 100 kujiandikisha na kadri mtu anavyozidi kujiandikisha anajitengeneza mazingira ya kushinda pesa taslimu kupitia droo ambayo itafanyika kila siku.
Hata hivyo KRG amewakikishia mashabiki zake pamoja na wakenya kwamba app hiyo imeidhinishwa na bodi inayodhibiti michezo ya kubashiri nchini, hivyo haihusiki kivyovyote na masuala ya kuwatapeli watu.
Maisha Poa ni app ambayo ipo chini ya kampuni ya Pepe Mtanii ambayo inalenga kuwasaidia vijana kuboresha maisha yao kupitia michongo mbali mbali.