Entertainment

KUNDI LA MABANTU LATUNUKIWA TUZO NA YOUTUBE KWA KUFIKISHA SUBSCRIBERS LAKI MOJA

KUNDI LA MABANTU LATUNUKIWA TUZO NA YOUTUBE KWA KUFIKISHA SUBSCRIBERS LAKI MOJA

Kundi la muziki nchini Tanzania Mabantu ambalo linaundwa na msanii Muuh na Twaah limetunukiwa tuzo ya Silver Play  Button na mtandao wa wa kustream muziki wa Youtube baada ya kundi hilo kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye mtandao huo.

Mabantu wametumia ukurasa wao wa instagram kuwashukuru mashabiki wao kwa kuwapa support kwenye muziki wao ambao unazidi kuwapa mafanikio makubwa

Channel ya youtube ya Mabantu ilifunguliwa rasmi Februari 14 mwaka wa 2018 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 9.2 huku ikiwa na subscribers 136, 000.

Itakumbukwa tuzo ya Silver Play Button huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa Youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja kwenye mtandao huo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *