
Kundi la muziki nchini Sauti Sol limepata ukosoaji mkubwa kutoka kwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukemea vikali mauji ya mwanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja Edwin Chiloba ambaye anadaiwa kuuwawa na mchumba wake Jackson Odhiambo.
Kwenye posti ya Sauti Sol kwenye mtandao wa Twitter iliyokuwa ikikashifu jamii kwa mauji ya jamaa huyo, Wakenya wameomekana kukerwa na kitendo cha kundi hilo kuwalaumu wanajamii kwa masuala yasiokuwa na msingi.
“It’s not the “Society” that did the heinous act. It’s her LGBT partner. Just a point of information.”, Aliandika mtumiaji mmoja wa Twitter
Baadhi ya wakenya wameitaka Sauti Sol kukoma kuihusisha jamii na mauji ya mwendazake Chiloba na badala yake waelekeze lawama zao kwa mtuhumiwa aliyetekeza ukatili huo kwani chanzo cha mauji hayo yanakwenda kinyume na maadili ya kiafrika.
“Why do gay people feel special. Let’s adhere to our traditions, norms and cultures. Before muanze kufundisha wengine tabia, jifundisheni”, Aliandika mtumiaji mmoja wa Twitter
Hata hivyo wamewatolea uvivu wasanii wa Sauti Sol kwa kutetea maslahi ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja huku wakisalia kimya kwa mauji ya kiholela ambayo yamekuwa yakifanyika nchini kila kuchao.
“Bwana sauti sol stop advocating for LGBTQ nonsense. Watu wanakufa kule Kisii daily, kule Baringo watu wanakufa daily . Why point out only this!,” Aliandika mtumiaji mmoja wa Twitter.