
Msanii nyota wa Bongofleva, Lava Lava, ametangaza rasmi ujio wa Extended Playlist (EP) yake mpya inayotarajiwa kuachiwa Ijumaa hii. Kazi hiyo mpya, inayokwenda kwa jina la Time, imebeba jumla ya nyimbo sita za moto, ikiwa na kolabo mbili za kuvutia kutoka kwa wasanii Yammi na Bill Nass.
EP hii inakuwa kazi yake ya kwanza tangu ajiondoe kwenye lebo ya WCB, hatua inayoashiria mwanzo mpya katika safari yake ya muziki akiwa msanii huru. Lava Lava amesema anatarajia mashabiki wataipokea kwa hamasa, akieleza kuwa “Time” ni mradi uliojaa ubunifu, hisia na ujumbe wa maisha.
Kwa mujibu wa taarifa, EP hiyo itapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mtandaoni kuanzia siku ya uzinduzi. Mashabiki wameshaanza kuonyesha shauku kubwa kupitia mitandao ya kijamii, wakisubiri kusikia ladha mpya kutoka kwa msanii huyo anayefahamika kwa sauti yake ya kipekee.