Today in History

LEO KATIKA HISTORIA FEBRUARI 28 MWAKA 2016 HAFLA YA UTOAJI TUZO ZA ACADEMY AWARDS ZILIFANYIKA HUKO LOS ANGELES

LEO KATIKA HISTORIA FEBRUARI 28 MWAKA 2016 HAFLA YA UTOAJI TUZO ZA ACADEMY AWARDS ZILIFANYIKA HUKO LOS ANGELES

Siku kama ya leo Februari 28 mwaka wa 2016 makala ya 88 ya tuzo za filamu nchini Marekani maarufu kama Academy Awards zilifanyika huko Los Angeles.

Tuzo hizo ambazo ziliendeshwa na Taasisi ya Academy of Motion Picture Arts and Sciences ziliandaliwa kwa ajili ya kutoa tuzo kwa waigizaji bora wa filamu mwaka wa 2015 kwenye vipengele 24.

Kwenye tuzo hizo filamu ya Spotlight ilishinda tuzo moja kwenye kipengele cha picha bora na kuifanya filamu ya pili kushinda tuzo hiyo baada ya filamu ya Greatest Show on Earth. Filamu ya Mad Max Fury Road ikashinda tuzo sita,The Revenant ikanyakua tuzo tatu kwenye kipengele cha Best Director, Best Actor na Best Actress.

Matukio ya tuzo hizo za Academy Awards maarufu kama Oscars yalipeperushwa mubashara kupitia runinga ya ABC nchini Marekani, matangazo yaliyotayarishwa na producer nguli nchini humo David Hill na Reginald Huldin.

Kwa upande wa kuongoza hafla hiyo Chris Rock alikuwa mfawidhi  kwa mara ya pili kwani pia amewahi kusimamia matangazo ya makala ya 77 ya Academy Awards mwaka wa 2005. Hata hivyo ni tuzo ambazo zilitazamwa na watu millioni  34.42 nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *