
Siku kama ya leo Novemba 11 mwaka wa 1990 alizaliwa mwanasoka kimataifa wa Uholanzi Georgino Wijnaldum ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Paris Saint-Germain inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa.
Jina lake halisi ni Georgino Gregion Emile na alizaliwa huko Rotterdam nchini Uholanzi ambako alianza soka mwaka wa 2007 kwenye klabu ya Feyernood ambapo aliisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la KNVB mwaka wa 2008 akiichezea klabu hiyo mechi 134 na kufunga magoli 23 kwa miaka mitano aliyoitumikia klabu ya Feyernood.
Baada ya kuigura klabu ya Feyernood mwaka wa 2011, Wijnaldum alijiunga na klabu ya PSV ambapo aliisaidia klabu hiyo kutwaaa kombe la Eridevese na KNVB akicheza mechi 109 na kutia kimiani magoli 40 kwa misimu minne aliyoitumikia klabu hiyo.
Mwaka wa 2015 Wijnaldum alitimukia nchini England na kudaka saini ya klabu ya Newcastle kwa pauni millioni 14.5 ambapo iliichezea klabu hiyo mechi 38 huku akifunga magoli 11 kwa msimu mmoja aliyoitumikia klabu ya Newcastle.
Baada ya klabu ya Newcastle kushushwa daraja mwaka wa 2016, Wijnaldum alijiunga na klabu ya Liverpool kwa pauni millioni 23 ambapo ameisaidia klabu hiyo mataji mengi ikiwemo Ligi kuu nchini England,taji la Klabu Bingwa Barani Ulaya na UEFA Super Cup.
Hata hivyo wijnaldum alifanikiwa kuichezea klabu ya Liverpool mechi 179 huku akifunga magoli 16 kwa misimu minne ambayo ameitumikia klabu hiyo.
Mwaka wa 2021 alitimukia nchini Ufaransa ambako alijiunga na klabu ya Paris Saint- Germain kwa uhamisho wa bure ambapo mpaka sasa ameichezea klabu hiyo mechi 12.
Katika ngazi ya kitaifa, Wijnaldum amewaikilisha timu ya taifa ya Uholanzi kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka wa 2014 na michuano ya Mataifa Bingwa Barani Ulaya mwaka wa 2018 ambapo kwa ujumla amechezea uholanzi mechi 83 huku kitia kimiani magoli 26 tangu mwaka wa 2011.