Today in History

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 9, ALIFARIKI DUNIA ALIYEKUWA MALKIA WA MUZIKI WA JAZZ BARANI AFRIKA, MIRIAM MAKEBA.

LEO KATIKA HISTORIA NOVEMBA 9, ALIFARIKI DUNIA ALIYEKUWA MALKIA WA MUZIKI WA JAZZ BARANI AFRIKA, MIRIAM MAKEBA.

Siku kama ya leo Novemba 9 mwaka wa 2008 alifariki dunia aliyekuwa Malkia muziki wa Jazz duniani na Balozi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa Mwanamama Miriam Makeba Maarufu kama Mama Afrika.

Makeba alizaliwa machi 8 mwaka wa 1932 huko  Johannesburg, Afrika ya Kusini na alifariki Novemba 9, mwaka wa 2008 akiwa na umri wa miaka 76.

Makeba alikuwa mwanzilishi wa nyimbo za Kiafrika na alisaidia kuleta mageuzi ya muziki wa Kiafrika, hadi akaitwa ‘Mama Afrika’ miaka ya 1960 na katika kipindi cha uhai wake alijipatia mafanikio makubwa kimuziki kwa kutoa albamu tisa na kuwa mshindi wa kwanza wa  tuzo ya grammy kutoka Afrika.

Hata hivyo Makeba ataendelea kukumbukwa kwa sauti yake yenye mvuto, ambayo inaelezwa kuwa haijawahi kusikika kutoka kwa mwanamuziki mwingine wa kike huko Afrika ya Kusini kupitia mikwaju yake kama pata pata,mailaka, aluta continua na hapo zamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *