
Msanii nyota wa Marekani, Lil Nas X, amejitokeza kupitia Instagram siku chache baada ya kukamatwa usiku mjini Los Angeles akiwa uchi na kudaiwa kushambulia polisi.
Katika ujumbe wake wa kwanza kwa mashabiki tangu tukio hilo, Lil Nas X amewahakikishia kwamba yuko salama. Hata hivyo, msanii huyo pia amekiri kuwa siku nne zilizopita zimekuwa za kutisha, akiashiria kwamba tukio hilo na mashtaka manne ya jinai anayokabiliana nayo si jambo dogo kwake.
Lil Nas X alishtakiwa kwa makosa manne ya jinai, ikiwemo tatu ya kushambulia maafisa wa polisi na moja ya kumpinga afisa wa utekelezaji wa sheria. Alikana mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya $75,000, pamoja na amri ya kuhudhuria vikao vya Narcotics Anonymous mara nne kwa wiki au kupata matibabu ya outpatient.
Kesi yake inatarajiwa kuendelea kusikilizwa kortini mwezi ujao baada ya kuachiwa kwa dhamana ya dola 75,000.