
Rapa Lil Wayne amezuiliwa kuingia nchini Uingereza kuelekea kwenye tamasha la Strawberries & Creem.
Waandaaji wa tamasha hilo wametoa taarifa isemayo, Lil Wayne amezuiliwa dakika za mwisho na wamesikitishwa na uamuzi huo wa wizara ya Mambo ya Ndani kwani Wizzy alikuwa msanii Kinara wa tamasha hilo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Uingereza ameiambia tovuti ya Rolling Stone kwamba, mtu yeyote ambaye aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 au zaidi, maombi yake kuingia nchini humo yatatupiliwa mbali.
Utakumbuka Mwaka 2007 Lil Wayne aliwahi kukamatwa kwa makosa ya silaha ambapo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja Jela lakini aliachiwa baada ya miezi 8 kutokana na mwenendo mzuri.