Sports news

Liverpool Yaangukia Pua Baada ya Kulazwa na Brighton 2-1

Liverpool Yaangukia Pua Baada ya Kulazwa na Brighton 2-1

Matumaini ya Liverpool kufuzu klabu bingwa Ulaya (Champions League) yamepata pigo kubwa baada ya kukubali kichapo cha 2-1 mikononi mwa Brighton & Hove Albion katika uwanja wa Amex.

Mshambuliaji mkongwe Danny Welbeck alikuwa mwiba mchungu kwa safu ya ulinzi ya Liverpool, akifunga mabao yote mawili ya wenyeji. Welbeck alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 14 kwa kichwa kikali akimalizia krosi ya Diego Gomez.

Ingawa Liverpool walisawazisha katika dakika ya 30 kupitia kwa beki wa kushoto Milos Kerkez, aliyenufaika na makosa ya Lewis Dunk, Welbeck alirejea tena dakika ya 56 kufunga bao la ushindi.

Kichapo hicho kinaiacha Liverpool katika nafasi ya tano na alama 49, ikizidiwa kete na timu zinazowania nafasi za klabu bingwa Ulaya. Kwa upande wao, Brighton wamepanda hadi nafasi ya nane na alama 43, wakizidi kuonyesha uimara wao msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *