
Msanii kutoka Tanzania Loui ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuwa na wimbo uliofikisha hadhi ya Platinum nchini Afrika Kusini.
Rekodi hiyo imewekwa kupitia wimbo wa SELEMA alioshirikiana na Musa Keys ambaye ni msanii na mtayarishaji kutoka nchini Afrika Kusini.
Kwenye mkutano na Waandishi wa habari, mwimbaji huyo ametuonesha Certificate ‘Plaque’ ambayo ametunukiwa na Recording Industry of South Africa (RISA) kwa mafanikio ya wimbo huo.
Mafanikio ya wimbo huo sio tu kwenye vituo vya Redio na Televisheni nchini Afrika Kusini bali ni hadi kwenye majukwaa makubwa ya kununua na kupakua muziki mtandaoni kama Spotify ambapo una zaidi ya Streams million 3.