Sports news

Luis Enrique aachana na timu ya Taifa ya Hispania

Luis Enrique aachana na timu ya Taifa ya Hispania

Kocha Luis Enrique ameachana na timu ya Taifa ya Hispania, ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kutolewa na Morocco katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayoendelea Qatar. Shirikisho la Soka Hispania ( RFEF) limethibitisha.

RFEF ilitoa taarifa ya kumshukuru Enrique kwa huduma yake na kueleza nia yake ya kuanzisha mradi mpya wa timu ya taifa.

Taarifa hiyo ilithibitisha kuwa mkataba wa Enrique unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu hautaongezwa tena.

Uhispania ilishindwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano hiyo iliyofanyika Qatar baada ya kushindwa na Morocco kwa mikwaju ya penalti siku ya Jumanne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *