Entertainment

MAANDY AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

MAANDY AACHIA TRACKLIST YA ALBUM YAKE MPYA

Msanii wa Kike nchini Maandy   hatimaye ameachia  rasmi Cover na orodha ya nyimbo zitakazopatikana kwenye album yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Frisky”

Kulingana na orodha ya nyimbo kupitia mtandao wa Instagram Maandy amethibitisha kuwa album yake ya Frisky inatarajiwa kuwa na nyimbo 12 ya moto, akiwa amewashirikisha wasanii watatu pekee ambao ni Breeder LW, Fena Gitu na Ndovu kuu.

Frisky kutoka kwa mtu mzima Maandy itaingia Sokoni Novemba 9  mwaka huu na itakuwa album yake ya pili baada ya kabaya iliyotoka mwaka wa 2019 ikiwa na jumla ua mikwaju 8 ya moto.

Tayari Maandy ameachia nyimbo mbili kutoka kwa album yake ya Frisky ambazo ni Hivi na Hivo na Sirudi home remix ambayo amemshirikisha Breeder LW na Ndovu Kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *